Saturday, June 30, 2018

IFAHAMU SHERIA YA MTOTO YA MWAKA 2OO9 (THE LAW OF THE CHILD ACT, 2009) [SEHEMU YA NANE]



SURA YA KUMI NA MBILI
HUDUMA YA MSAADA KWA MTOTO KUTOKA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MTAA
Wajibu wa Mamlaka ya Serikali za Mtaa
Mtoto anafanyiwa nini na Mamlaka ya Serikali za Mtaa?
(i) Mamlaka ya Serikali ya Mtaa itakuwa na wajibu wa kulinda na kukuza ustawi wa mtoto katika eneo la mamlaka hiyo.
(ii) Ofisa wa Ustawi wa Jamii katika mamlaka ya Serikali ya Mtaa atatimiza kazi zake kuhusiana na ustawi wa mtoto. Atasaidiwa na maofisa wa Serikali ya Mtaa kama mamlaka inavyoweza kuamua.
(iii) Mamlaka ya Serikali ya Mtaa kwa kupitia Ofisa wa Ustawi wa Jamii itatoa ushauri kwa wazazi, walezi na ndugu na watoto kwa madhumuni ya kukuza upatano kati yao.73
(iv) Mamlaka ya Serikali ya Mtaa itakuwa na wajibu wa kutunza Rejesta ya Watoto wenye kuweza kudhurika zaidi katika eneo lake. Watatoa msaada pale inapowezekana ili kuwawezesha watoto kukua kwa hadhi na heshima baina ya watoto wengine, kukuza vipaji na uwezo wa kujitegemea.
(v) Kila mamlaka ya Serikali ya Mtaa katika eneo lake itatakiwa kutoa msaada na mahali pa kuishi kwa mtoto anayeonekana kwa mamlaka hiyo kuhitaji msaada. Mtoto atakayehitaji msaada anaweza kuwa amepotea au kutelekezwa au anatafuta hifadhi.
(vi) Kila mamlaka ya Serikali ya Mtaa itafanya kazi na polisi kwa kila jitihada kuwatafuta wazazi, walezi au ndugu wa mtoto aliyepotea, aliyetelekezwa na kumrudisha mtoto mahali alipokuwa akiishi.
Serikali ya Mtaa ikishindwa kuwapata wazazi au ndugu, itapeleka suala hili kwa Ofisa wa Ustawi wa Jamii.
(vii) Ofisa wa Ustawi wa Jamii na polisi katika eneo la mamlaka ya Serikali ya Mtaa watapeleleza kesi zote za kukiuka au kuvunjwa kwa haki za watoto.
74
Taarifa ya Kuvunjwa kwa Haki za Watoto
Mwanajumuiya katika jamii ana wajibu gani kwa mtoto?
(i) Mwanajumuiya yeyote ana wajibu wa kutoa taarifa kwa mamlaka ya Serikali ya Mtaa kwamba haki za mtoto zinavunjwa. Taarifa iwe na ushahidi kwamba mzazi, mlezi au ndugu anayemlea mtoto ana uwezo lakini anakataa au hajali kutoa chakula, malazi, haki ya kucheza au kupumzika, mavazi, huduma ya kitabibu au elimu.
(ii) Ofisa wa Ustawi wa Jamii, baada ya kupokea taarifa, atamuita mzazi au ndugu ambaye taarifa ilitolewa dhidi yake, ili kujadili suala hilo. Maamuzi yatafanywa na Ofisa wa Ustawi wa Jamii kwa ajili ya ustawi wa mtoto.
(iii) Pale ambapo mtu ambaye taarifa ilitolewa dhidi yake anakataa kutekeleza maamuzi yaliyotolewa na Ofisa wa Ustawi wa Jamii, ofisa huyo wa Ustawi wa Jamii atapeleka suala hilo mahakamani.
Mahakama itasikiliza shauri na kuhukumu suala hilo. Inaweza:
(a) Kutoa faraja au amri iliyoombwa kama mazingira yanavyohitaji; na
(b) Ikatoa amri iliyoombwa dhidi ya mzazi, na kumuamuru mzazi kutoa dhamana kama ziada ya faraja iliyotolewa ili kutoa huduma stahili na ulinzi kwa kusaini na kuahidi kumpatia mtoto lolote au mahitaji yote.
(iv) Katika sheria hii, Mahakama ya kwanza itakuwa mahakama ya kuanzia kwa masuala yote chini ya sehemu hii. Rufaa kutoka mahakama hii itafuata utaratibu wa kawaida wa rufaa.
(v) Mtu yeyote anayevunja kifungu kidogo cha (i) anatenda kosa. Akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini au kutumikia kifungo kwa muda wa miezi mitatu au vyote kwa pamoja.
76
Uchunguzi wa Makosa Dhidi ya Mtoto
Ulinzi wa mtoto unafatiliwa namna gani? Na nani?
(i) Pale ambapo Ofisa wa Ustawi wa Jamii, kwa sababu za msingi, anahisi mtoto anatendewa vibaya au anahitaji huduma na ulinzi, anaweza kuingia na kukagua nyumba ambamo mtoto anatunzwa ili kuchunguza. Katika kufanya hilo, ataambatana na ofisa wa polisi.
(ii) Baada ya kuchunguza na kuonekana kuwa mtoto ametendewa vibaya au anahitaji huduma ya haraka na ulinzi, Ofisa wa Ustawi wa Jamii atamtoa mtoto na kumuweka sehemu ya usalama kwa muda usiozidi siku saba. Atamtoa mtoto akiwa na ofisa wa polisi.
(iii) Mtoto anapokuwa amewekwa sehemu nyingine, au ametolewa ili kupata huduma ya ulinzi, Ofisa wa Ustawi wa Jamii atampeleka mtoto mahakamani ndani ya siku kumi na nne kwa ajili ya amri nyingine kutolewa.
(iv) Mpaka mahakama itakapoamua suala hili, mahakama inaweza kumweka mtoto kwenye makazi yaliyoidhinishwa au chini ya malezi ya Ofisa wa Ustawi wa Jamii au kwa mtu yeyote anayefaa.
78
SURA YA KUMI NA TATU
MTOTO MWENYE MGOGORO NA SHERIA

Mahakama ya Watoto
Kuanzishwa kwa mahakama ya watoto
Mahakama ya Watoto ina faida gani?
(i) Kutakuwa na mahakama ya Watoto itakayokuwa na madhumuni ya kusikiliza na kuamua masuala yanayohusu watoto.
(ii) Mahakama ya Watoto itaongozwa na Hakimu Mkazi.

Uwezo wa Mahakama ya Watoto
Mahakama ya Watoto inafanya nini?
(i) Mahakama ya Watoto itakuwa na uwezo wa kusikiliza na kuamua:-
(a) Mashtaka ya jinai dhidi ya watoto.
(b) Maombi yanayohusu matunzo, kukimu na kuwalinda watoto.
(ii) Mahakama ya Watoto itakuwa pia na uwezo na mamlaka iliyopewa na sheria nyingine yoyote iliyoandikwa.
(iii) Mahakama ya Watoto, pale inapowezekana, itakaa katika jengo jingine tofauti na jengo la kawaida kwa ajili ya kusikiliza kesi dhidi ya watu wazima.

Taratibu katika Mahakama ya Watoto
Je, taratibu za mahakama zinamlindaje mtoto akishtakiwa?
(i) Utaratibu wa kuendesha mashauri katika mahakama ya watoto utafuata kanuni zitakazotengenezwa na Jaji Mkuu. Lakini, kwa vyovyote vile, utazingatia masharti yafuatayo:
(a) Mahakama ya Watoto itakaa mara kwa mara kufuatana na ulazima;
(b) Mashauri yataendeshwa kwa faragha;
(c) Mashauri yatakuwa ya kawaida. Uchunguzi wa mashauri utafanywa kwa njia ambayo uchunguzi hautampinga mtoto.
(d) Ofisa Ustawi wa Jamii atakuwepo wakati wa kuendesha mashauri.
(e) Ni haki ya mzazi, mlezi au ndugu kuwepo.
(f) Mtoto atakuwa na haki ya kuwa na ndugu wa karibu au kuwakilishwa na wakili.
(g) Haki ya kukata rufaa itafafanuliwa kwa mtoto ili aielewe.
(h) Mtoto atakuwa na haki ya kutoa ufafanuzi na maoni.
(ii) Pamoja na wajumbe na maofisa wa Mahakama ya Watoto, watu walio orodheshwa hapa chini wanaweza kuruhusiwa na mahakama wakati inapokaa kusikiliza shauri:
8(a) Wahusika wa shauri lililopo mahakamani, mawakili wao, mashahidi, wahusika wengine wa moja kwa moja na shauri lililopo mahakamani.
(b) Mtu mwingine yeyote ambaye mahakama inaweza kumruhusu awepo mahakamani.

Mwenendo wa Shauri katika Mahakama ya Watoto
(i) Mahakama ya Watoto inaposikiliza tuhuma dhidi ya mtoto, itakaa katika jengo au chumba kingine tofauti na jengo au chumba ambacho mashauri ya kawaida ya mahakama husikilizwa. Kama mtoto anashtakiwa pamoja na mtu mwingine ambaye si
mtoto, mashauri yatasikilizwa kwenye chumba cha kawaida cha mahakama.
(ii) Pale ambapo shauri linaendelea kusikilizwa na ikaonekana kwa mahakama kuwa mtu aliyeshtakiwa ni mtoto, mahakama itasitisha mwenendo wa mashtaka na kumpeleka mtoto kwenye Mahakama ya Watoto.
(iii) Pale ambapo shauri linaendelea kusikilizwa na ikaonekana kwa mahakama kuwa mtu aliyeshtakiwa ni mtu mzima, mahakama itaendelea kusikiliza shauri. Maamuzi yatafanywa kulingana na Sheria ya Mahakama za Mahakimu au Sheria ya Mwenendo
wa Mashtaka, kama itakavyokuwa.
82
Dhamana kwa Ajili ya Mtoto
Je, mtoto akikamatwa, anatendewa nini? Nani anaweza kumwekea dhamana?
(i) Pale ambapo mtoto anakamatwa kwa hati au bila hati ya kukamata, na hawezi kupelekwa mahakamani mara moja, ofisa mkuu wa kituo cha polisi ambako amepelekwa atamwachia mtoto huru. Mtoto anaweza kujidhamini yeye mwenyewe,
au kudhaminiwa na wazazi, walezi au ndugu au bila kuwa na wadhamini. Isipokuwa:
(a) Kama mashtaka ni ya mauaji au kosa ambalo adhabu yake ni kifungo kwa kipindi kinachozidi miaka saba.
(b) Kama ni lazima kwa ajili ya ustawi wa mtoto kumtoa ili asihusiane na mtu asiyefaa; au
(c) Ofisa ana sababu kuamini kuwa kumtoa mtoto kutavunja haja ya kutenda haki.
Uhusiano na watu wazima mtoto anapokuwa kizuizini
(i) Ofisa wa Polisi atafanya mpango kwa ajili ya kuzuia, kama inawezekana kufanyika, mtoto aliye kizuizini asihusiane na mtu mzima anayetuhumiwa kutenda kosa, isipokuwa kama ni ndugu.
83
Mahakama ya Watoto inaweza kusikiliza mashauri yote isipokuwa kama ni mashtaka ya mauaji
(i) Ofisa wa Polisi hatampeleka mtoto mahakamani isipokuwa kama upelelezi umekamilika. Au kama kosa linahitaji apelekwe mahakamani.
(ii) Mtoto anapopelekwa mahakama ya watoto kwa kosa lolote lile, mahakama itasikiliza shauri hilo siku hiyohiyo, isipokuwa kwa kosa la mauaji.

HITIMISHO
Ni matumaini yangu kuwa mara baada ya kuisoma sheria hii ya mtoto ya mwaka 2009, kila mmoja wetu atahakikisha anamlinda mtoto ikiwa ni pamoja na kumpatia haki zake zote za msingi.
Sehemu kubwa ya makala hii imechukuliwa kutoka kwenye chapisho la HakiElimu linaloelezea sheria ya mtoto kwa lugha rahisi.

Tafadhali soma Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 (The Law of the Child Act, 2009) hapa chini:


No comments:

Post a Comment

FAHAMU KUHUSU MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs)


SHULE INAYOTOA MICHEZO KAMA HII INAFAA KWA MZAZI NA MLEZI KUPELEKA MTOTO WAKE