SURA YA TANO
UZAO
Maombi ya Nasaba
Kama baba wa mtoto hajulikani, nani
anaweza kuomba uthibitisho wa uzao?
(i) Wafuatao wanaweza kuomba
mahakamani amri ya kuthibitisha uzao wa mtoto:
(a) Mtoto;
(b) Mzazi wa mtoto;
(c) Mlezi wa mtoto;
(d) Ofisa wa Ustawi wa Jamii; au
(e) Kwa ruhusa rasmi ya mahakama, mtu
yeyote mwenye kuvutiwa na mtoto.
(ii) Ni wakati gani maombi
yanaweza kufanywa
mahakamani ?
(a) Kabla mtoto hajazaliwa;
(b) Baada ya kifo cha baba au mama wa
mtoto;
(c) Kabla mtoto hajafikisha umri wa miaka kumi na nane. Inawezekana pia, kwa ruhusa rasmi ya mahakama, kuomba amri ya kuthibitisha uzao baada ya mtoto kufikisha umri wa miaka kumi na nane.
Ushahidi wa Nasaba
(i). Ushahidi wa uzao wa mtoto
unatokana na nini?
(a) Ndoa yoyote iliyofungwa kwa
kufuata Sheria ya Ndoa;
(b) Jina la mzazi kuingizwa katika
rejesta ya vizazi inayotunzwa na Msajili Mkuu;
(c) Kufanywa kwa sherehe ya kimila na
baba wa mtoto;
(d) Kutambuliwa na jamii kwa uzao
huo: na
(e) Matokeo ya vipimo vya vinasaba.
Vipimo vya Nasaba ni nini?
Hivi ni vipimo ambavyo vinatoa
ushahidi thabiti juu ya uzao wa mtoto. Baba anayedhaniwa kuwa baba mzazi anapimwa
vipimo vya nasaba ili kuwa na uhakika kwamba yeye ndiye baba mzazi. Nasaba
hupatikana katika kiini cha seli hai na huwa na taarifa za urithi kutoka kwa
mzazi kwenda kwa mtoto. Taarifa za nasaba ndizo pekee zenye kutoa ukweli
usiopingika kuhusu uzao wa mtoto.
40
Vipimo vya Kidaktari
(i) Mahakama inaweza kutoa amri, kwa
anayesemekana kuwa ni baba mzazi wa mtoto, kupeleka vipimo vya kidaktari. Kwa
kutegemea na ushahidi utakaopatikana kutokana na vipimo, mahakama itatoa amri
kama inavyoona inafaa.
(ii) Pamoja na vipimo vya kidaktari,
pale ambapo ushahidi wa mama au ushahidi mwingine wowote unaojitegemea haulingani/haufanani
na ushahidi uliopatikana kutokana na vipimo, mahakama yenyewe, inaweza kuamuru
vipimo vya vinasaba vifanywe kwa nia ya kuthibitisha baba mzazi wa mtoto.
Au, maombi ya vipimo vya kinasaba
yanaweza kupelekwa mahakamani.
(iii) Mahakama itaamua na kutoa amri
nani atalipia gharama kuhusiana na vipimo vya vinasaba.
(iv) Pale mahakama inapotoa amri
kuhusu baba mzazi, baba huyu atachukua majukumu kwa mtoto kama vile anavyowajibika
kwa mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa. Mtoto naye, kwa kuzingatia dini ya baba mzazi,
atakuwa na haki zote kutoka kwa baba pamoja na haki ya urithi.
42
SURA YA SITA
UANGALIZI NA NJIA YA KUMTEMBELEA
MTOTO
Nani anaweza kuwa mwangalizi wa
mtoto?
(i) Mzazi, mlezi au ndugu anayemtunza
mtoto anaweza kuomba mahakamani kuwa mwangalizi wa mtoto.
(ii) Mahakama inaweza kutoa amri ya
kuishi na mtoto kwa mwombaji kuwa mwangalizi, kwa masharti itakayoona yanafaa.
Hili litategemea mwenendo wa maombi ya kuthibitisha uzao wa mtoto.
(iii) Mahakama inaweza, wakati wowote,
kufuta amri ya kuishi na mtoto kama mwangalizi kwa mtu na kumpatia mtu mwingine
majukumu hayo.
Majukumu hayo yanaweza pia yakapatiwa
makazi yaliyoidhinishwa au taasisi, kama mahakama ikiona ni lazima.
(iv) Katika kufikia maamuzi ya kutoa
amri ya kuwa mwangalizi wa mtoto au kufuta amri hiyo, mahakama itazingatia
kwanza furaha na amani ya mtoto.
43
Kumtembelea mtoto
Mzazi, mlezi au ndugu ambaye
amefutiwa amri ya kuwa mwangalizi wa mtoto anaweza kuomba mahakamani kupata
nafasi ya kumtembelea mtoto kwa vipindi maalumu.
Uamuzi juu ya Kumtembelea Mtoto
(i) Mahakama itazingatia furaha na
amani ya mtoto na umuhimu wa mtoto kuwa na mama yake wakati inapotoa amri ya uangalizi
wa mtoto na kumtembelea mtoto.
(ii) Wakati wa kutoa amri ya
uangalizi, mahakama inazingatia nini?
(a) Haki za mtoto;
(b) Umri na jinsia ya mtoto;
(c) Kama inafaa mtoto kuwa na wazazi,
isipokuwa kama mtoto atanyimwa haki zake za kuwa na wazazi. Au, kama wazazi
wataendelea kuzivunja haki za mtoto.
(d) Maoni ya mtoto, kama maoni hayo
yametolewa kwa uhuru.
(e) Kwamba inafaa kuwaweka ndugu
pamoja;
(f) Hitaji la kuwepo mwendelezo wa
matunzo na udhibiti wa mtoto; na
( g) Jambo lolote ambalo mahakama
itaona linafaa.
Kumuondoa Mtoto Kinyume cha Sheria
(i) Mtu yeyote atakuwa anatenda kosa,
kama atamwondoa mtoto kutoka kwa mtu anayeishi naye kihalali, makazi
yaliyoidhinishwa au taasisi, kinyume cha sheria.
SURA YA SABA
MATUNZO
Ni nani wanaweza kuomba kumtunza
mtoto?
(i) Watu wafuatao wanaweza kuomba
mahakamani amri ya kukimu mtoto:-
(a) Mzazi wa mtoto;
(b) Mlezi wa mtoto
(c) Mtoto mwenyewe, kwa kumtumia
rafiki wa karibu;
(d) Ofisa wa Ustawi wa Jamii
(e) Ndugu wa mtoto.
(ii) Maombi ya kukimu mtoto yanaweza
kufanywa dhidi ya mtu yeyote anayestahili kumtunza mtoto, au kwa madhumuni ya
kuchangia kwa ajili ya ustawi na matunzo ya mtoto.
Amri ya kukimu mtoto dhidi ya
anayesemekana ni baba mzazi wa mtoto
(i) Maombi ya amri ya kukimu mtoto
yanaweza kufanywa mahakama ni dhidi ya baba anayesemekana kuwa baba mzazi wa
mtoto.
46
Maombi ya kukimu yanaweza kufanywa na
nani?
(a) Na Mama anayetarajia kujifungua
wakati wowote kabla ya mtoto kuzaliwa;
(b) Na mzazi ambaye amri ya uzao
imetolewa dhidi yake na mahakama.
Ni wakati gani maombi ya kukimu mtoto
yanaweza kufanywa?
(c) Wakati wowote ndani ya miezi
ishirini na nne (miaka miwili) baada ya kuzaliwa mtoto;
(d) Wakati wowote baada ya mtoto
kuzaliwa, na baada ya kuthibitisha kwamba mwanamume anayesemekana kuwa ni baba
wa kibaiolojia wa mtoto amelipa hela kwa ajili ya kumkimu mtoto ndani ya miezi
ishirini na nne baada ya mtoto kuzaliwa.
(e) Wakati wowote ndani ya miezi
ishirini na nne baada ya baba mzazi wa mtoto kurudi ndani ya Tanzania Bara,
baada ya kuthibitika kwamba aliacha kuishi Tanzania kabla au baada ya mtoto
kuzaliwa.
(ii) Mahakama itakataa kutoa amri ya
kukimu mtoto chini ya kifungu cha (i) isipokuwa ikiridhika kwamba:
(a) Kuna sababu ya maana kuamini
kwamba mwanamume anayesemekana ni baba wa mtoto, kweli ni baba wa mtoto, na
kwamba maombi ya matunzo yamefanywa kwa nia njema wala si kwa lengo la kuogofya
na kulazimisha malipo kwa nguvu; na
(b) Mwanamume anayesemekana kuwa ni
baba wa mtoto ameombwa na mwombaji au mtu mwingine kwa niaba ya mwombaji kutoa matunzo
ya mtoto naye amekataa au amepuuzia kutoa matunzo au ametoa kidogo.
Uamuzi kwa ajili ya Amri ya Kukimu
Mtoto
(i) Mahakama itaangalia mambo
yafuatayo inapotoa amri ya malipo ya matunzo:
(a) Kipato na utajiri wa wazazi wote
wa mtoto au wa mtu ambaye kisheria anawajibika kutoa matunzo ya mtoto;
(b) Kama kipato cha mtu anayewajibika
kutoa
matunzo ya mtoto kikididimia.
(c) Majukumu ya kifedha mtu aliyonayo
kwa matunzo ya watoto wengine;
(d) Gharama za maisha za eneo ambapo
mtoto anaishi; na
(e ) Haki za mtoto chini ya sheria
hii.
48
(ii) Mtu yeyote ambaye anamlea mtoto
anayehusika na amri ya kukimu mtoto anastahili kupokea na kusimamia amri ya
mahakama ya kukimu mtoto.
(iii) Pale mzazi, mlezi au mtu yeyote
anayemlea mtoto anapopoteza sifa za kuwa mtu anayefaa, mahakama iliyopo katika
eneo analoishi mtoto inaweza kumteua mtu mwingine awe mlezi wa mtoto. Mtu huyu atasimamia
amri ya kukimu mtoto na atatimiza majukumu yake kama vile aliteuliwa na
mahakama tangu awali.
Muda wa Amri ya Kukimu Mtoto
(i) Amri ya kukimu mtoto iliyotolewa
na mahakama itadumu mpaka mtoto anapofikisha umri wa miaka kumi na nane. Au
itadumu hadi apate ajira inayompatia kipato. Au amekufa kabla ya kutimiza umri
wa miaka kumi na nane.
Mwendelezo wa Amri ya Kukimu
(i) Mahakama inaweza kuendelea
kutekeleza amri ya kukimu mtoto baada ya mtoto kutimiza umri wa miaka kumi na nane.
Amri ya kukimu itaendelea kama mtoto bado anaendelea na masomo au mafunzo,
licha ya muda wa ukomo kama ilivyoainishwa katika sheria hii.
(ii) Maombi chini ya fungu hili
yanaweza kuletwa na mzazi wa mtoto, mtu yeyote anayemlea mtoto, au mtoto
mwenyewe.
(iii) Mtu yeyote mwingine anaweza
kupeleka maombi mahakami kutekeleza amri ya kukimu mtoto ndani ya siku arobaini
na tano baada ya amri kutolewa au
kuwa tayari kwa utekelezaji.
Je, mzazi ambaye haishi na mtoto
anaruhusiwa kumwona?
Mzazi ambaye haishi na mtoto
ataruhusiwa kumtembelea mtoto. Jambo hili halizuiwi na amri ya kuthibitisha uzao,
uangalizi, kumtembelea mtoto au ya kukimu mtoto iliyotolewa na mahakama dhidi
yake.
No comments:
Post a Comment