Saturday, June 30, 2018

IFAHAMU SHERIA YA MTOTO YA MWAKA 2OO9 (THE LAW OF THE CHILD ACT, 2009) [SEHEMU YA NANE]



SURA YA KUMI NA MBILI
HUDUMA YA MSAADA KWA MTOTO KUTOKA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MTAA
Wajibu wa Mamlaka ya Serikali za Mtaa
Mtoto anafanyiwa nini na Mamlaka ya Serikali za Mtaa?
(i) Mamlaka ya Serikali ya Mtaa itakuwa na wajibu wa kulinda na kukuza ustawi wa mtoto katika eneo la mamlaka hiyo.
(ii) Ofisa wa Ustawi wa Jamii katika mamlaka ya Serikali ya Mtaa atatimiza kazi zake kuhusiana na ustawi wa mtoto. Atasaidiwa na maofisa wa Serikali ya Mtaa kama mamlaka inavyoweza kuamua.
(iii) Mamlaka ya Serikali ya Mtaa kwa kupitia Ofisa wa Ustawi wa Jamii itatoa ushauri kwa wazazi, walezi na ndugu na watoto kwa madhumuni ya kukuza upatano kati yao.73
(iv) Mamlaka ya Serikali ya Mtaa itakuwa na wajibu wa kutunza Rejesta ya Watoto wenye kuweza kudhurika zaidi katika eneo lake. Watatoa msaada pale inapowezekana ili kuwawezesha watoto kukua kwa hadhi na heshima baina ya watoto wengine, kukuza vipaji na uwezo wa kujitegemea.
(v) Kila mamlaka ya Serikali ya Mtaa katika eneo lake itatakiwa kutoa msaada na mahali pa kuishi kwa mtoto anayeonekana kwa mamlaka hiyo kuhitaji msaada. Mtoto atakayehitaji msaada anaweza kuwa amepotea au kutelekezwa au anatafuta hifadhi.
(vi) Kila mamlaka ya Serikali ya Mtaa itafanya kazi na polisi kwa kila jitihada kuwatafuta wazazi, walezi au ndugu wa mtoto aliyepotea, aliyetelekezwa na kumrudisha mtoto mahali alipokuwa akiishi.
Serikali ya Mtaa ikishindwa kuwapata wazazi au ndugu, itapeleka suala hili kwa Ofisa wa Ustawi wa Jamii.
(vii) Ofisa wa Ustawi wa Jamii na polisi katika eneo la mamlaka ya Serikali ya Mtaa watapeleleza kesi zote za kukiuka au kuvunjwa kwa haki za watoto.
74
Taarifa ya Kuvunjwa kwa Haki za Watoto
Mwanajumuiya katika jamii ana wajibu gani kwa mtoto?
(i) Mwanajumuiya yeyote ana wajibu wa kutoa taarifa kwa mamlaka ya Serikali ya Mtaa kwamba haki za mtoto zinavunjwa. Taarifa iwe na ushahidi kwamba mzazi, mlezi au ndugu anayemlea mtoto ana uwezo lakini anakataa au hajali kutoa chakula, malazi, haki ya kucheza au kupumzika, mavazi, huduma ya kitabibu au elimu.
(ii) Ofisa wa Ustawi wa Jamii, baada ya kupokea taarifa, atamuita mzazi au ndugu ambaye taarifa ilitolewa dhidi yake, ili kujadili suala hilo. Maamuzi yatafanywa na Ofisa wa Ustawi wa Jamii kwa ajili ya ustawi wa mtoto.
(iii) Pale ambapo mtu ambaye taarifa ilitolewa dhidi yake anakataa kutekeleza maamuzi yaliyotolewa na Ofisa wa Ustawi wa Jamii, ofisa huyo wa Ustawi wa Jamii atapeleka suala hilo mahakamani.
Mahakama itasikiliza shauri na kuhukumu suala hilo. Inaweza:
(a) Kutoa faraja au amri iliyoombwa kama mazingira yanavyohitaji; na
(b) Ikatoa amri iliyoombwa dhidi ya mzazi, na kumuamuru mzazi kutoa dhamana kama ziada ya faraja iliyotolewa ili kutoa huduma stahili na ulinzi kwa kusaini na kuahidi kumpatia mtoto lolote au mahitaji yote.
(iv) Katika sheria hii, Mahakama ya kwanza itakuwa mahakama ya kuanzia kwa masuala yote chini ya sehemu hii. Rufaa kutoka mahakama hii itafuata utaratibu wa kawaida wa rufaa.
(v) Mtu yeyote anayevunja kifungu kidogo cha (i) anatenda kosa. Akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini au kutumikia kifungo kwa muda wa miezi mitatu au vyote kwa pamoja.
76
Uchunguzi wa Makosa Dhidi ya Mtoto
Ulinzi wa mtoto unafatiliwa namna gani? Na nani?
(i) Pale ambapo Ofisa wa Ustawi wa Jamii, kwa sababu za msingi, anahisi mtoto anatendewa vibaya au anahitaji huduma na ulinzi, anaweza kuingia na kukagua nyumba ambamo mtoto anatunzwa ili kuchunguza. Katika kufanya hilo, ataambatana na ofisa wa polisi.
(ii) Baada ya kuchunguza na kuonekana kuwa mtoto ametendewa vibaya au anahitaji huduma ya haraka na ulinzi, Ofisa wa Ustawi wa Jamii atamtoa mtoto na kumuweka sehemu ya usalama kwa muda usiozidi siku saba. Atamtoa mtoto akiwa na ofisa wa polisi.
(iii) Mtoto anapokuwa amewekwa sehemu nyingine, au ametolewa ili kupata huduma ya ulinzi, Ofisa wa Ustawi wa Jamii atampeleka mtoto mahakamani ndani ya siku kumi na nne kwa ajili ya amri nyingine kutolewa.
(iv) Mpaka mahakama itakapoamua suala hili, mahakama inaweza kumweka mtoto kwenye makazi yaliyoidhinishwa au chini ya malezi ya Ofisa wa Ustawi wa Jamii au kwa mtu yeyote anayefaa.
78
SURA YA KUMI NA TATU
MTOTO MWENYE MGOGORO NA SHERIA

Mahakama ya Watoto
Kuanzishwa kwa mahakama ya watoto
Mahakama ya Watoto ina faida gani?
(i) Kutakuwa na mahakama ya Watoto itakayokuwa na madhumuni ya kusikiliza na kuamua masuala yanayohusu watoto.
(ii) Mahakama ya Watoto itaongozwa na Hakimu Mkazi.

Uwezo wa Mahakama ya Watoto
Mahakama ya Watoto inafanya nini?
(i) Mahakama ya Watoto itakuwa na uwezo wa kusikiliza na kuamua:-
(a) Mashtaka ya jinai dhidi ya watoto.
(b) Maombi yanayohusu matunzo, kukimu na kuwalinda watoto.
(ii) Mahakama ya Watoto itakuwa pia na uwezo na mamlaka iliyopewa na sheria nyingine yoyote iliyoandikwa.
(iii) Mahakama ya Watoto, pale inapowezekana, itakaa katika jengo jingine tofauti na jengo la kawaida kwa ajili ya kusikiliza kesi dhidi ya watu wazima.

Taratibu katika Mahakama ya Watoto
Je, taratibu za mahakama zinamlindaje mtoto akishtakiwa?
(i) Utaratibu wa kuendesha mashauri katika mahakama ya watoto utafuata kanuni zitakazotengenezwa na Jaji Mkuu. Lakini, kwa vyovyote vile, utazingatia masharti yafuatayo:
(a) Mahakama ya Watoto itakaa mara kwa mara kufuatana na ulazima;
(b) Mashauri yataendeshwa kwa faragha;
(c) Mashauri yatakuwa ya kawaida. Uchunguzi wa mashauri utafanywa kwa njia ambayo uchunguzi hautampinga mtoto.
(d) Ofisa Ustawi wa Jamii atakuwepo wakati wa kuendesha mashauri.
(e) Ni haki ya mzazi, mlezi au ndugu kuwepo.
(f) Mtoto atakuwa na haki ya kuwa na ndugu wa karibu au kuwakilishwa na wakili.
(g) Haki ya kukata rufaa itafafanuliwa kwa mtoto ili aielewe.
(h) Mtoto atakuwa na haki ya kutoa ufafanuzi na maoni.
(ii) Pamoja na wajumbe na maofisa wa Mahakama ya Watoto, watu walio orodheshwa hapa chini wanaweza kuruhusiwa na mahakama wakati inapokaa kusikiliza shauri:
8(a) Wahusika wa shauri lililopo mahakamani, mawakili wao, mashahidi, wahusika wengine wa moja kwa moja na shauri lililopo mahakamani.
(b) Mtu mwingine yeyote ambaye mahakama inaweza kumruhusu awepo mahakamani.

Mwenendo wa Shauri katika Mahakama ya Watoto
(i) Mahakama ya Watoto inaposikiliza tuhuma dhidi ya mtoto, itakaa katika jengo au chumba kingine tofauti na jengo au chumba ambacho mashauri ya kawaida ya mahakama husikilizwa. Kama mtoto anashtakiwa pamoja na mtu mwingine ambaye si
mtoto, mashauri yatasikilizwa kwenye chumba cha kawaida cha mahakama.
(ii) Pale ambapo shauri linaendelea kusikilizwa na ikaonekana kwa mahakama kuwa mtu aliyeshtakiwa ni mtoto, mahakama itasitisha mwenendo wa mashtaka na kumpeleka mtoto kwenye Mahakama ya Watoto.
(iii) Pale ambapo shauri linaendelea kusikilizwa na ikaonekana kwa mahakama kuwa mtu aliyeshtakiwa ni mtu mzima, mahakama itaendelea kusikiliza shauri. Maamuzi yatafanywa kulingana na Sheria ya Mahakama za Mahakimu au Sheria ya Mwenendo
wa Mashtaka, kama itakavyokuwa.
82
Dhamana kwa Ajili ya Mtoto
Je, mtoto akikamatwa, anatendewa nini? Nani anaweza kumwekea dhamana?
(i) Pale ambapo mtoto anakamatwa kwa hati au bila hati ya kukamata, na hawezi kupelekwa mahakamani mara moja, ofisa mkuu wa kituo cha polisi ambako amepelekwa atamwachia mtoto huru. Mtoto anaweza kujidhamini yeye mwenyewe,
au kudhaminiwa na wazazi, walezi au ndugu au bila kuwa na wadhamini. Isipokuwa:
(a) Kama mashtaka ni ya mauaji au kosa ambalo adhabu yake ni kifungo kwa kipindi kinachozidi miaka saba.
(b) Kama ni lazima kwa ajili ya ustawi wa mtoto kumtoa ili asihusiane na mtu asiyefaa; au
(c) Ofisa ana sababu kuamini kuwa kumtoa mtoto kutavunja haja ya kutenda haki.
Uhusiano na watu wazima mtoto anapokuwa kizuizini
(i) Ofisa wa Polisi atafanya mpango kwa ajili ya kuzuia, kama inawezekana kufanyika, mtoto aliye kizuizini asihusiane na mtu mzima anayetuhumiwa kutenda kosa, isipokuwa kama ni ndugu.
83
Mahakama ya Watoto inaweza kusikiliza mashauri yote isipokuwa kama ni mashtaka ya mauaji
(i) Ofisa wa Polisi hatampeleka mtoto mahakamani isipokuwa kama upelelezi umekamilika. Au kama kosa linahitaji apelekwe mahakamani.
(ii) Mtoto anapopelekwa mahakama ya watoto kwa kosa lolote lile, mahakama itasikiliza shauri hilo siku hiyohiyo, isipokuwa kwa kosa la mauaji.

HITIMISHO
Ni matumaini yangu kuwa mara baada ya kuisoma sheria hii ya mtoto ya mwaka 2009, kila mmoja wetu atahakikisha anamlinda mtoto ikiwa ni pamoja na kumpatia haki zake zote za msingi.
Sehemu kubwa ya makala hii imechukuliwa kutoka kwenye chapisho la HakiElimu linaloelezea sheria ya mtoto kwa lugha rahisi.

Tafadhali soma Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 (The Law of the Child Act, 2009) hapa chini:


IFAHAMU SHERIA YA MTOTO YA MWAKA 2OO9 (THE LAW OF THE CHILD ACT, 2009) [SEHEMU YA SABA]



SURA YA KUMI
KURITHI MALI
Kugawa Mali bila Wasia
Je, mtoto aliyeasiliwa atarithi mali zipi?
(i) Pale mzazi wa kuasili anapofariki bila kuacha wasia, mali zake zinakuwa mali za mtoto wa kuasili, kama vile mtoto amezaliwa na wazazi wa kuasili.
(ii) Kwa ajili ya kuondoa utata, mtoto wa kuasili hatastahili kurithi mali kama wazazi wake wa kibaiolojia wakifa bila kuacha wasia.
Kugawa Mali kwa Wasia
(i) Mgawanyo unaofanywa baada ya tarehe ya amri ya kuasili, iwe mali halisi au binafsi, iwe au isiwe kwa maandishi, itazingatia:
(a) Maelezo yoyote yenye marejeo, yaliyo wazi au kwa kuhisi, yanayohusu mtoto wa mzazi wa kuasili, yanamhusu pia mtoto wa kuasili, isipokuwa kama itaonyeshwa vinginevyo.
(b) Pale ambapo mgao ulifanywa na mzazi wa kuasili kabla ya tarehe ya kutolewa amri ya kuasili, na mtoto wa kuasili hakutajwa katika mgao huo, mtoto wa kuasili anaweza kuomba mahakamani ili mgao huo uweze kubadilishwa, ili naye ahusishwe katika mgao.
(c) Marejeo yoyote kwa wazazi wa mtoto wa kuasili katika wasia, hayatatafsiriwa kumhusisha mtoto aliyeasiliwa, isipokuwa kama kutakuwa na nia ya kufanya hivyo.
(d) Marejeo yoyote kwa ndugu wa mzazi wa kuasili, hayatatafsiriwa kuwa yanarejea kwa mtu huyo kama vile ni ndugu wa mtoto aliyeasiliwa, isipokuwa kama kutakuwa na nia ya kufanya hivyo.
(ii) Mgao katika wasia unaofanywa kabla ya tarehe ya amri ya kuasili hautachukuliwa kama vile umefanywa baada ya tarehe ya amri ya kuasili. Kiambatisho cha wasia cha tarehe kabla ya amri ya kuasili hakiwezi kukubalika.
(iii) Mgao, lina maana ya kuhamisha masilahi katika mali kwa hati yoyote, iwe kwa watu walio hai, au kwa wasia, ikiwa ni pamoja na kiambatisho cha wasia.
63
SURA YA KUMI NA MOJA
AJIRA YA MTOTO
Haki ya Mtoto Kufanya Kazi
(i) Mtoto atakuwa na haki ya kufanya kazi nyepesi.
(ii) Pamoja na kwamba mtoto ana haki ya kufanya kazi nyepesi, umri wa chini wa kuajiri mtoto utakuwa miaka kumi na nne.

Kazi nyepesi ni zipi?
(iii) Kazi nyepesi” itahusisha kazi ambayo haiwezi kuwa na madhara kwa afya ya mtoto, au kwa maendeleo yake. Kazi hiyo haitamzuia au haitaathiri mahudhurio ya mtoto ya shule, kushiriki katika shughuli za kujiendeleza kiufundi au programu ya mafunzo au uwezo wa mtoto kunufaika na kazi za shule.

Kukataza Kazi za Kiunyonyaji
(i) Mtu hataruhusiwa kumuajiri au kumshughulisha mtoto katika aina yoyote ya kazi itakayomnyonya mtoto.
(ii) Bila kupingana na kifungu hiki cha sheria, kila mwajiri atahakikisha kuwa kila mtoto aliyeajiriwa kihalali na kulingana na sheria hii, analindwa.
Mtoto ana haki ya kulindwa dhidi ya kutengwa au matendo yoyote yanayoweza kuwa na athari mbaya kwake kwa kuzingatia umri na uwezo wake.

(iii) Nini maana ya kazi za kinyonyaji?
Kazi itakuwa ni ya kinyonyaji iwapo:
(a) Inamnyima mtoto kuwa na afya njema au maendeleo;
(b) Ni ya muda zaidi ya saa sita kwa siku;
(c) Haifai kwa umri wake; au
(d) Mtoto hapati malipo ya kutosha
(iv) Mtu yeyote anayevunja sheria katika kifungu hiki anatenda kosa. Akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki moja au kutumikia kifungo kwa muda wa miezi mitatu au vyote kwa pamoja.

Ni katika kazi zipi mtoto hawezi kuajiriwa?

Kukataza Kazi za Usiku
(i) Bila kupingana na sheria hii, mtoto hataajiriwa au kuhusishwa katika mkataba wa huduma ambayo itamuhitaji mtoto afanye kazi usiku.
(ii) “Kazi ya usiku” ni kazi inayohusu utendaji unaohitaji mtoto awe kazini kati ya saa mbili jioni na saa kumi na mbili asubuhi.
(iii) Mtu yeyote anayevunja sheria katika kifungu hiki anatenda kosa. Akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki moja au kutumikia kifungo kwa muda wa miezi mitatu au vyote kwa pamoja.
66
Kukataza Ajira ya Lazima
(i) Mtu yeyote atakayemshawishi, atakayempeleka, atakayemtaka au atakayemlazimisha mtoto kufanya kazi kwa lazima anatenda kosa.
(ii) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, ‘ajira ya muda” inahusisha kazi ya kitumwa au kazi yoyote inayofanyika kwa vitisho vya adhabu. Ajira ya muda haihusishi kazi za kawaida za kijamii, kazi ndogondogo za huduma kwa jamii zinazofanywa na wanajumuiya kwa manufaa ya jamii.
(iii) Mtu yeyote anayevunja sheria katika kifungu hiki anatenda kosa. Akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili au kutumikia kifungo cha muda wa miezi sita au vyote kwa pamoja.

Haki ya Kulipwa Ujira
(i) Mtoto ana haki ya kulipwa ujira sawa na thamani ya kazi aliyofanya.
(ii) Licha ya sheria kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Kazi na Uhusiano wa Kikazi, mwajiri yeyote ambaye anakiuka sheria katika kifungu hiki anatenda kosa.
67
Ajira ya Hatari
(i) Siyo halali kisheria kumuajiri au kumhusisha mtoto kwenye kazi ya hatari.

Ajira za hatari ni zipi?
(ii) Kazi ya hatari ni kazi yoyote inayoweza kuleta hatari kwa afya, usalama na maadili ya mtoto.
(iii) Kazi ya hatari itahusisha:-
(a) Kwenda baharini;
(b) Kufanya kazi migodini au kuchimba na kupasua kokoto;
(c) Kubeba mizigo mizito;
(d) Kufanya kazi katika viwanda vya uzalishaji ambako kemikali zinatengenezwa au kutumika;
(e) Kufanya kazi sehemu ambako mashine zinatumika; na
(f) Kufanya kazi sehemu za baa, hoteli au sehemu nyingine za starehe.
(iv) Pamoja na kwamba kazi za hatari zimeainishwa na kuzuiwa, sheria yoyote iliyoandikwa inayosimamia mafunzo inaweza kumruhusu mtoto:
(a) Kuingia katika merikebu ili ahudhurie mafunzo kama sehemu ya mafunzo ya mtoto;
(b) Katika kiwanda au mgodi, kama kazi ni sehemu ya mafunzo ya mtoto;
(c ) Katika sehemu yoyote ya kazi kwa masharti kwamba afya, usalama, na maadili ya mtoto vitalindwa na mtoto amepata au anapata maelekezo maalumu, au mafunzo yanayoendana na kazi au shughuli hiyo.

Kumtumia Mtoto kwa Shughuli za Kikahaba
(i) Mtoto hataajiriwa katika kazi yoyote au biashara inayomweka mtoto katika mazingira ya ngono, iwe kwa malipo au la;
(ii) Kwa kuondoa utata, itakuwa ni kukiuka sheria kwa mtu yoyote kutumia:
(a) Ushawishi au kumlazimisha mtoto ashiriki katika vitendo vya ngono;
(b) Watoto katika vitendo au shughuli zozote za umalaya;
(c) Watoto katika kutengeneza picha au maandishi yenye kutia ashiki.
(iii) Mtu yeyote anayevunja sheria katika kifungu hiki anatenda kosa. Akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni moja na isiyozidi shilingi milioni tano au kutumikia kifungo kwa muda usiopungua mwaka mmoja na usiozidi miaka
ishirini au vyote kwa pamoja.

Sheria juu ya kazi za hatari itatumika sehemu gani?
(i) Kwa kuzuia utata, sehemu hii itatumika kwa ajira katika sekta rasmi na isiyo rasmi.
(ii) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (i), Ofisa wa Kazi, katika muda muafaka, ataingia katika nyumba au sehemu ya nyumba na kufanya ukaguzi kama ataona ni lazima, ili kujiridhisha kwamba sheria katika sehemu hii inatekelezwa.
(iii) Neno “nyumba” lina maana ya nyumba, shirika, kampuni, ofisi, uwanja, shamba, eneo; na inahusisha chombo, merikebu, gari na ndege.
70
Usajili wa Mtoto katika Sehemu za Kazi
Je, taarifa zinazohusu mtoto katika sehemu ya kazi ni zipi?
(i) Mwajiri, katika sehemu za kazi, atatunza rejesta ya watoto walioajiriwa naye, tarehe za kuzaliwa kwao, kama zinafahamika au umri unaodhaniwa kuwa ndio umri wao, kama tarehe zao za kuzaliwa hazijulikani.
(ii) Shughuli za kikazi ni shughuli nyingine ambazo si za kibiashara au kilimo. Shughuli za kikazi zinajumuisha:
(a) Migodi, machimbo ya mawe, na kazi nyingine za kuchimba madini kutoka ardhini.
(b) Shughuli ambazo kutokana nazo, vitu mbalimbali vinatengenezwa, vinabadilishwa,
vinasafishwa, vinakarabatiwa, vinapambwa, vinaboreshwa, vinatwaliwa kwa kuuzwa,
vinavunjwa au kuharibiwa, au ambako vitu vinabadilishwa. Zinajumuisha shughuli za
kujenga merikebu au shughuli za kufua, kubadili na kusambaza umeme au nishati ya
aina yoyote.
(c) Shughuli za kusafirisha abiria au bidhaa kwa barabara au reli pamoja na kushughulikia bidhaa katika gati, kikwezo, ghala na uwanja wa ndege.
71
Utekelezaji wa Sheria
Sheria ya ajira kwa watoto inafuatiliwa na nani? Wakati gani?
(i) Ofisa wa Kazi atafanya uchunguzi wowote kama anaona ni lazima ili kujiridhisha kwamba sheria katika sehemu hii kuhusu ajira ya watoto zinatekelezwa kwa hakika.
(ii) Ofisa wa Kazi anaweza kumusaili mtu yeyote kama ni lazima.
(iii) Pale ambapo Ofisa wa Kazi kwa busara zake ameridhika kwamba sheria katika kifungu hiki haitekelezwi, atatoa amri ya kutokutekelezwa kwa sheria katika ajira. Ofisa wa Kazi atapeleka ripoti kwa Ofisa Ustawi wa Jamii na kituo cha polisi kilicho karibu. Ofisa wa Ustawi wa Jamii na polisi watafanya upelelezi na kuchukua hatua zinazofaa ili kumlinda mtoto.

FAHAMU KUHUSU MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs)


SHULE INAYOTOA MICHEZO KAMA HII INAFAA KWA MZAZI NA MLEZI KUPELEKA MTOTO WAKE