SURA YA KUMI NA MBILI
HUDUMA YA MSAADA KWA MTOTO KUTOKA
MAMLAKA YA SERIKALI ZA MTAA
Wajibu wa Mamlaka ya Serikali za Mtaa
Mtoto anafanyiwa nini na Mamlaka ya
Serikali za Mtaa?
(i) Mamlaka ya Serikali ya Mtaa
itakuwa na wajibu wa kulinda na kukuza ustawi wa mtoto katika eneo la mamlaka
hiyo.
(ii) Ofisa wa Ustawi wa Jamii katika
mamlaka ya Serikali ya Mtaa atatimiza kazi zake kuhusiana na ustawi wa mtoto.
Atasaidiwa na maofisa wa Serikali ya Mtaa kama mamlaka inavyoweza kuamua.
(iii) Mamlaka ya Serikali ya Mtaa kwa
kupitia Ofisa wa Ustawi wa Jamii itatoa ushauri kwa wazazi, walezi na ndugu na
watoto kwa madhumuni ya kukuza upatano kati yao.73
(iv) Mamlaka ya Serikali ya Mtaa
itakuwa na wajibu wa kutunza Rejesta ya Watoto wenye kuweza kudhurika zaidi katika
eneo lake. Watatoa msaada pale inapowezekana ili kuwawezesha watoto kukua kwa
hadhi na heshima baina ya watoto wengine, kukuza vipaji na uwezo wa
kujitegemea.
(v) Kila mamlaka ya Serikali ya Mtaa
katika eneo lake itatakiwa kutoa msaada na mahali pa kuishi kwa mtoto anayeonekana
kwa mamlaka hiyo kuhitaji msaada. Mtoto atakayehitaji msaada anaweza kuwa amepotea
au kutelekezwa au anatafuta hifadhi.
(vi) Kila mamlaka ya Serikali ya Mtaa
itafanya kazi na polisi kwa kila jitihada kuwatafuta wazazi, walezi au ndugu wa
mtoto aliyepotea, aliyetelekezwa na kumrudisha mtoto mahali alipokuwa akiishi.
Serikali ya Mtaa ikishindwa kuwapata
wazazi au ndugu, itapeleka suala hili kwa Ofisa wa Ustawi wa Jamii.
(vii) Ofisa wa Ustawi wa Jamii na
polisi katika eneo la mamlaka ya Serikali ya Mtaa watapeleleza kesi zote za
kukiuka au kuvunjwa kwa haki za watoto.
74
Taarifa ya Kuvunjwa kwa Haki za
Watoto
Mwanajumuiya katika jamii ana wajibu
gani kwa mtoto?
(i) Mwanajumuiya yeyote ana wajibu wa
kutoa taarifa kwa mamlaka ya Serikali ya Mtaa kwamba haki za mtoto zinavunjwa.
Taarifa iwe na ushahidi kwamba mzazi, mlezi au ndugu anayemlea mtoto ana uwezo
lakini anakataa au hajali kutoa chakula, malazi, haki ya kucheza au kupumzika,
mavazi, huduma ya kitabibu au elimu.
(ii) Ofisa wa Ustawi wa Jamii, baada
ya kupokea taarifa, atamuita mzazi au ndugu ambaye taarifa ilitolewa dhidi
yake, ili kujadili suala hilo. Maamuzi yatafanywa na Ofisa wa Ustawi wa Jamii
kwa ajili ya ustawi wa mtoto.
(iii) Pale ambapo mtu ambaye taarifa
ilitolewa dhidi yake anakataa kutekeleza maamuzi yaliyotolewa na Ofisa wa
Ustawi wa Jamii, ofisa huyo wa Ustawi wa Jamii atapeleka suala hilo mahakamani.
Mahakama itasikiliza shauri na
kuhukumu suala hilo. Inaweza:
(a) Kutoa faraja au amri iliyoombwa
kama mazingira yanavyohitaji; na
(b) Ikatoa amri iliyoombwa dhidi ya
mzazi, na kumuamuru mzazi kutoa dhamana kama ziada ya faraja iliyotolewa ili
kutoa huduma stahili na ulinzi kwa kusaini na kuahidi kumpatia mtoto lolote au
mahitaji yote.
(iv) Katika sheria hii, Mahakama ya
kwanza itakuwa mahakama ya kuanzia kwa masuala yote chini ya sehemu hii. Rufaa
kutoka mahakama hii itafuata utaratibu wa kawaida wa rufaa.
(v) Mtu yeyote anayevunja kifungu
kidogo cha (i) anatenda kosa. Akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini
isiyopungua shilingi elfu hamsini au kutumikia kifungo kwa muda wa miezi mitatu
au vyote kwa pamoja.
76
Uchunguzi wa Makosa Dhidi ya Mtoto
Ulinzi wa mtoto unafatiliwa namna
gani? Na nani?
(i) Pale ambapo Ofisa wa Ustawi wa
Jamii, kwa sababu za msingi, anahisi mtoto anatendewa vibaya au anahitaji huduma
na ulinzi, anaweza kuingia na kukagua nyumba ambamo mtoto anatunzwa ili kuchunguza.
Katika kufanya hilo, ataambatana na ofisa wa polisi.
(ii) Baada ya kuchunguza na kuonekana
kuwa mtoto ametendewa vibaya au anahitaji huduma ya haraka na ulinzi, Ofisa wa
Ustawi wa Jamii atamtoa mtoto na kumuweka sehemu ya usalama kwa muda usiozidi
siku saba. Atamtoa mtoto akiwa na ofisa wa polisi.
(iii) Mtoto anapokuwa amewekwa sehemu
nyingine, au ametolewa ili kupata huduma ya ulinzi, Ofisa wa Ustawi wa Jamii
atampeleka mtoto mahakamani ndani ya siku kumi na nne kwa ajili ya amri
nyingine kutolewa.
(iv) Mpaka mahakama itakapoamua suala
hili, mahakama inaweza kumweka mtoto kwenye makazi yaliyoidhinishwa au chini ya
malezi ya Ofisa wa Ustawi wa Jamii au kwa mtu yeyote anayefaa.
78
SURA YA KUMI NA TATU
MTOTO MWENYE MGOGORO NA SHERIA
Mahakama ya Watoto
Kuanzishwa kwa mahakama ya watoto
Mahakama ya Watoto ina faida gani?
(i) Kutakuwa na mahakama ya Watoto
itakayokuwa na madhumuni ya kusikiliza na kuamua masuala yanayohusu watoto.
(ii) Mahakama ya Watoto itaongozwa na
Hakimu Mkazi.
Uwezo wa Mahakama ya Watoto
Mahakama ya Watoto inafanya nini?
(i) Mahakama ya Watoto itakuwa na
uwezo wa kusikiliza na kuamua:-
(a) Mashtaka ya jinai dhidi ya
watoto.
(b) Maombi yanayohusu matunzo, kukimu
na kuwalinda watoto.
(ii) Mahakama ya Watoto itakuwa pia
na uwezo na mamlaka iliyopewa na sheria nyingine yoyote iliyoandikwa.
(iii) Mahakama ya Watoto, pale
inapowezekana, itakaa katika jengo jingine tofauti na jengo la kawaida kwa ajili
ya kusikiliza kesi dhidi ya watu wazima.
Taratibu katika Mahakama ya Watoto
Je, taratibu za mahakama zinamlindaje
mtoto akishtakiwa?
(i) Utaratibu wa kuendesha mashauri
katika mahakama ya watoto utafuata kanuni zitakazotengenezwa na Jaji Mkuu.
Lakini, kwa vyovyote vile, utazingatia masharti yafuatayo:
(a) Mahakama ya Watoto itakaa mara
kwa mara kufuatana na ulazima;
(b) Mashauri yataendeshwa kwa
faragha;
(c) Mashauri yatakuwa ya kawaida.
Uchunguzi wa mashauri utafanywa kwa njia ambayo uchunguzi hautampinga mtoto.
(d) Ofisa Ustawi wa Jamii atakuwepo
wakati wa kuendesha mashauri.
(e) Ni haki ya mzazi, mlezi au ndugu
kuwepo.
(f) Mtoto atakuwa na haki ya kuwa na
ndugu wa karibu au kuwakilishwa na wakili.
(g) Haki ya kukata rufaa
itafafanuliwa kwa mtoto ili aielewe.
(h) Mtoto atakuwa na haki ya kutoa
ufafanuzi na maoni.
(ii) Pamoja na wajumbe na maofisa wa
Mahakama ya Watoto, watu walio orodheshwa hapa chini wanaweza kuruhusiwa na
mahakama wakati inapokaa kusikiliza shauri:
8(a) Wahusika wa shauri lililopo mahakamani, mawakili wao, mashahidi, wahusika wengine
wa moja kwa moja na shauri lililopo mahakamani.
(b) Mtu mwingine yeyote ambaye
mahakama inaweza kumruhusu awepo mahakamani.
Mwenendo wa Shauri katika Mahakama ya
Watoto
(i) Mahakama ya Watoto inaposikiliza
tuhuma dhidi ya mtoto, itakaa katika jengo au chumba kingine tofauti na jengo
au chumba ambacho mashauri ya kawaida ya mahakama husikilizwa. Kama mtoto anashtakiwa
pamoja na mtu mwingine ambaye si
mtoto, mashauri yatasikilizwa kwenye
chumba cha kawaida cha mahakama.
(ii) Pale ambapo shauri linaendelea
kusikilizwa na ikaonekana kwa mahakama kuwa mtu aliyeshtakiwa ni mtoto, mahakama
itasitisha mwenendo wa mashtaka na kumpeleka mtoto kwenye Mahakama ya Watoto.
(iii) Pale ambapo shauri linaendelea
kusikilizwa na ikaonekana kwa mahakama kuwa mtu aliyeshtakiwa ni mtu mzima,
mahakama itaendelea kusikiliza shauri. Maamuzi yatafanywa kulingana na Sheria ya
Mahakama za Mahakimu au Sheria ya Mwenendo
wa Mashtaka, kama itakavyokuwa.
82
Dhamana kwa Ajili ya Mtoto
Je, mtoto akikamatwa, anatendewa
nini? Nani anaweza kumwekea dhamana?
(i) Pale ambapo mtoto anakamatwa kwa
hati au bila hati ya kukamata, na hawezi kupelekwa mahakamani mara moja, ofisa
mkuu wa kituo cha polisi ambako amepelekwa atamwachia mtoto huru. Mtoto anaweza
kujidhamini yeye mwenyewe,
au kudhaminiwa na wazazi, walezi au
ndugu au bila kuwa na wadhamini. Isipokuwa:
(a) Kama mashtaka ni ya mauaji au
kosa ambalo adhabu yake ni kifungo kwa kipindi kinachozidi miaka saba.
(b) Kama ni lazima kwa ajili ya
ustawi wa mtoto kumtoa ili asihusiane na mtu asiyefaa; au
(c) Ofisa ana sababu kuamini kuwa
kumtoa mtoto kutavunja haja ya kutenda haki.
Uhusiano na watu wazima mtoto anapokuwa
kizuizini
(i) Ofisa wa Polisi atafanya mpango
kwa ajili ya kuzuia, kama inawezekana kufanyika, mtoto aliye kizuizini asihusiane
na mtu mzima anayetuhumiwa kutenda kosa, isipokuwa kama ni ndugu.
83
Mahakama ya Watoto inaweza kusikiliza
mashauri yote isipokuwa kama ni mashtaka ya mauaji
(i) Ofisa wa Polisi hatampeleka mtoto
mahakamani isipokuwa kama upelelezi umekamilika. Au kama kosa linahitaji
apelekwe mahakamani.
(ii) Mtoto anapopelekwa mahakama ya
watoto kwa kosa lolote lile, mahakama itasikiliza shauri hilo siku hiyohiyo,
isipokuwa kwa kosa la mauaji.
HITIMISHO
Ni matumaini yangu kuwa mara baada ya kuisoma sheria hii ya mtoto ya mwaka 2009, kila mmoja wetu atahakikisha anamlinda mtoto ikiwa ni pamoja na kumpatia haki zake zote za msingi.
Sehemu kubwa ya makala hii imechukuliwa kutoka kwenye chapisho la HakiElimu linaloelezea sheria ya mtoto kwa lugha rahisi.
Tafadhali soma Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 (The Law of the Child Act, 2009) hapa chini: